SiasaUkraine
Zelensky akerwa na viongozi kutohudhuria mkutano wa Uswisi
2 Juni 2024Matangazo
Zelensky ameyasema hayo leo Jumapili katika kongamano la usalama nchini Singapore, ambako ameomba msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine.
"Tunasikitishwa kwamba baadhi ya viongozi wa dunia bado hawajathibitisha kushiriki katika mkutano huo wa amani. Kwa bahati mbaya, kuna majaribio ya kuvuruga mkutano huo. Hatutaki kuamini kwamba hii ni tamaa ya mamlaka ya ukiritimba duniani, kunyima jumuiya ya kimataifa fursa ya kuamua juu ya vita na amani na kuacha mamlaka hii mikononi mwa mmoja au wawili.", alisema Zelensky.
Rais Zelensky amesema ziara yake huko Singapore ni katika umuhimu wa kupata ungwaji mkono wa nchi za Asia-Pacifiki kwa ajili ya mkutano ujao wa siku mbili wa amani ya Ukraine huko Uswisi katikati mwa mwezi huu.