1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky afanya mazungumzo na Biden mjini Washington

22 Septemba 2023

Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky amekutana na rais wa Marekani Joe Biden mjini Washington kwa mazungumzo juu ya uvamizi wa Urusi nchini mwake.

https://p.dw.com/p/4WfuS
Volodmyr Zelensky I Joe Biden
Rais wa Ukraine Volodmyr Zelensky na rais wa Marekani Joe BidenPicha: Drew Angerer/Getty Images

Katika mazungumzo ya viongozi hao yaliyofanyika kwenye ikulu ya Marekani, Rais Biden ametoa ahadi ya kuipa Ukraine silaha mpya za ulinzi wa anga.

Zelensky anafanya ziara hiyo nchini Marekani wakati ambapo wajumbe wahafidhina wa chama cha Republican wanaitaka serikali iwe na uangalifu juu ya misaada ya Marekani inayotolewa kwa Ukraine.Watu wawili wafariki nchini Ukraine kufuatia mashambulizi ya Urusi

Wabunge wa chama hicho cha Republican wameelezea mashaka juu ya misaada hiyo.Rais Zelensky kuzuru Marekani wiki ijayo

Kwa upande wake Zelensky ametahadharisha kwamba nchi yake inaweza kushindwa vita kati yake na Urusi iwapo wabunge wa chama cha Republican watapunguza msaada wa kijeshi wa mamilioni ya dola kwa Ukraine.