1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky adai kuwa serikali yake imejiandaa kuishinda Urusi

19 Septemba 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema serikali yake imetayarisha mpango wake wa ushindi wa kumaliza vita na Urusi, ambao amesema wataujadili na rais wa Marekani Joe Biden.

https://p.dw.com/p/4kpJ1
Ukraine Kiev | Hotuba ya video na Volodymyr Zelenskyj
Volodymyr Zelensky kwenye hotuba yake kupitia video.Picha: president.gov.ua/en

Hata hivyo vita hivyo vilivyodumu kwa zaidi ya miezi 30 vinaendelea kurindima. Urusi ilishambulia miundombinu ya nishati katika mkoa wa kaskazini-mashariki mwa Ukraine wa Sumy.Shirika la Kimataifala Nishati limesema hivi leo kuwa majira ya baridi yatakuwa changamoto kwa gridi ya nishati ya Ukraine kufuatia mitambo mingi kuharibiwa.