1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelenskiy: Jeshi la Ukraine linapiga hatua Kursk

29 Agosti 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa wanajeshi wake wanapiga hatua na kuchukua udhibiti wa maeneo zaidi kufuatia uvamizi wao katika mkoa wa Kursk nchini Urusi.

https://p.dw.com/p/4k2P5
Ukraine Region Volyn | Selenskij inspiziert Befestigungsanlagen an Grenze zu Weißrussland
Picha: UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS/REUTERS

Hata hivyo Zelensky hakutoa maelezo zaidi, lakini akawashukuru wanajeshi wake na kusema kwamba hatua hiyo itasaidia kuwarejesha nyumbani watu wao kutoka kwenye utumwa wa Urusi.

Wanajeshi wa Ukraine walivamia ardhi ya Urusi katika shambulio la ghafla huko Kursk mnamo Agosti 6. Moscow na Kiev zimekuwa zikishambuliana vikali katika siku za hivi karibuni.

Vyacheslav Gladkov, Gavana wa Belgorod ambalo ni eneo la Urusi linalopakana pia na Ukraine amesema kuna ripoti kwamba jeshi la Ukraine lilijaribu kuvuka mpaka na kuingia eneo hilo.