Zelenskiy atafuta msaada na silaha kanda ya Balkan
28 Februari 2024Rais Zelenskiyamekuwa akizunguka dunia katika wiki za hivi karibuni kutafuta uungwaji mkono kwa nchi yake inayokabiliwa na mzozo, huku wanajeshi wa Ukraine wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa risasi na wakipambana kuzuia maendeleo ya kijeshi ya Urusi ardhini.
Aliwasili Albania Jumanne jioni na hii leo amekutana mjini Tirana na viongozi kadhaa kutoka kanda nzima wanaohudhuria mkutano wa kilele wa Ukraine na Mataifa ya Kusini-Mashariki mwa Ulaya - ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika taifa hilo la Balkan tangu uvamizi wa Urusi Februari 2022.
Mkutano huo wa kilele katika mji mkuu wa Albania, Tirana unakuja wakati Kyiv inajaribu kuboresha uwezo wake wa ulinzi ili kuvishinda vikosi vya Urusi wakati ambapo msaada wa Marekani umesimma kufuatia mkwamo bungeni.
Soma pia:Marekani: Hatuna mpango wa kupeleka wanajeshi nchini Ukraine
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo wa kilele, Zelenskiy aliauambia ujumbe wa ngazi za juu kutoka Albania, Serbia, Macedonia Kaskazini, Montenegro, Croatia na Moldova, kwamba wanataka kushirikiana na mataifa yao katika uzalishaji na washirika wote wa nchi yake.
Ushirikiano wa kutengeneza silaha
Hata hivyo sio mataifa yate yanayoshiriki mkutano huo yanaiunga mkono kikamilifu Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi. Mshirika wa Krelim Serbia, ndio nchi pekee ya Ulaya ambayo imekataa kukubaliana na vikwazo vya Umoja wa Ulaya kufuatia uvamizi kamili wa Urusi, na rais wake Alexander Vucic ameyataja mazugumzo hayo kuwa magumu.
Soma pia:Macron: Hatufuti uwezekano wa kupeleka wanajeshi Ukraine
Zelenskiy amependekeza kuandaa kongamano la ulinzi kati ya Ukraine na mataifa ya Balkan mjini Kyiv au mji mkuu wowote wa taifa la Balkan ili kukuza ushirikiano katika nyanja ya zana za kivita, akirudia mipango kama hiyo iliyofanyika mwaka jana kwa kuzihusisha kampuni za silaha za Uingereza na Marekani.
Wakati huo huo, Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen amependekza kutumia fedha za Urusi zilizozuwiliwa kwa ajili ya jeshi la Ukraine.