1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Zambia yaingia mkataba wa kulipa madeni yake

14 Oktoba 2023

Wizara ya fedha ya Zambia imesema imekubali kuingia katika mkataba wa kulipa madeni yake na wakopeshaji wa kigeni.

https://p.dw.com/p/4XXS2

Katika mkutano wa kila mwaka wa shirika la IMF na Benki ya Dunia, huko Marrakesh wizara ya fedha ya Zambia imesema hatua hiyo itatoa unafuu wa kifedha kwa nchi hiyo, ambayo mnamo 2020 ilikuwa taifa la kwanza barani Afrika kushindwa kulipa madeni yake baada ya janga la Uviko.

Zambia ilikuwa imefikia makubaliano ya msingi na wakopeshaji wake, ambao ni pamoja na China na mataifa ya Magharibi, kuhusu dola bilioni 6.3 za deni lake la mwezi Juni, lakini mpango huo ulikuwa bado haujakamilika.

Soma zaidi: Yellen azuru Zambia kujadilia madeni ya China, afya ya umma

Hata hivyo IMF imesema kwamba mkataba huo unatarajiwa kusainiwa hivi karibuni.

Waziri wa Fedha wa Zambia Situmbeko Musokotwane amesema serikali yake imejitolea kujikwamua kutoka kwenye madeni yanayozidi kudhoofisha uchumi. Amesema baada ya kuyafanyia kazi madeni hayo, serikali ya Zambia itaachilia rasilimali ambazo ni muhimu kuziwekeza katika ajenda ya maendeleo.