IOM: Zaidi ya watu milioni 7 ni wakimbizi wa ndani Sudan
6 Septemba 2023Matangazo
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia uhamiaji IOM limesema watu takriban milioni 7.1 wamekuwa wakimbizi wa ndani nchini Sudan kutokana na vita vilivyoanza mnamo Aprili mwaka huu. Shirika hilo limesema zaidi ya asilimia 50 ni watu wapya waliolazimika kuyahama makazi yao kutokana na vita hivyo.
Shirika la IOM limesema sasa linatarajia watu milioni 1.8 kuikimbia Sudan kufikia mwisho wa mwaka huu na limetoa wito wa msaada wa dola bilioni moja kuwasaidia huku kukiwa na ripoti za ongezeko la kasi ya maambukizi ya magonjwa na vifo.