1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

IOM: Zaidi ya watu 6,300 wayakimbia makazi yao, Haiti

7 Oktoba 2024

Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM) limesema watu wasiopungua 70, wameuawa nchini Haiti na wengine takriban 6,300 wameyakimbia makazi yao kutokana na mashambulizi.

https://p.dw.com/p/4lU0Y
Machafuko nchini Haiti
Watu wakichoma moto takataka karibu na miili ya watu10 kutoka magenge ya wahalifu waliouawa katika makabiliano na vikosi vya usalama mjini Port-au-Prince Picha: Guerinault Louis/Anadolu/picture alliance

Kulingana na Shirika la IOM, mashambulizi hayo yalifanywa katikati mwa nchi hiyo na genge la watu wenye silaha.

Ofisi ya kamishna wa Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema katika taarifa yake kwamba ilishtushwa mno na mashambulizi ya magenge ya wahalifu yaliyofanyika siku ya Alhamisi.

Umoja wa Ulaya pia umelaani ghasia hizo katika taarifa yake ambayo imesema mashambulio hayo yanaashiria kuongezeka tena kwa hali mbaya inayowakabili watu wa Haiti.