Zaidi ya watu 40 wahofiwa kufariki Mashariki mwa Kongo
1 Septemba 2023Jeshi la Kongo lilitawanya kwa nguvu maandamano hayo mjini Goma baada ya kanda ya video iliyoonesha shambulizi dhidi ya afisa wa polisi kusambazwa katika mitandao ya kijamii. Hata hivyo kanda hiyo haikuweza kuthibitishwa. Mamlaka inasema kuwa afisa huyo aliuawa kwa kupigwa mawe na kwamba waandamanaji sita waliuawa jeshi lilipoingilia.
Hospitali zimekuwa zikipokea malori yaliobeba maiti
Lakini maafisa hao wawili wa jeshi waliozungumza kwa sharti la kutotambulishwa, wamesema hospitali zimekuwa zikipokea malori kadhaa yaliobeba maiti tangu maandamano hayo kuanza na kusema idadi hiyo ni zaidi ya watu 40.
Soma pia:Watu wasiopungua kumi wauawa katika maandamano mjini Goma
Chanzo kimoja cha Umoja wa Mataifa, kimesema wanachunguza madai ya vifo zaidi ya hamsini baada ya wanajeshi hao kuwazuia waandamanaji waliokuwa wamekusanyika kanisani kabla ya kuanza kwa maandamano hayo.
Hata hivyo msemaji wa jeshi la Kongo Luteni Kanali Guillaume Ndjike amekanusha ripoti hiyo na kusema ni watu saba pekee waliopoteza maisha.