1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Zaidi ya 100,000 wakimbia mapigano chini ya wiki moja Kongo

8 Januari 2025

Mapigano katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamesababisha zaidi ya watu 100,000 kugeuka wakimbizi ndani ya wiki moja tu iliyopita.

https://p.dw.com/p/4owDV
DR Kongo Kibumba 2022 | Waasi wa M23
Waasi wa M23 wamechukuwa maeneo makubwa Mashariki mwa KongoPicha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, baina ya tarehe 1 na 3 Januari, mapigano makali kati ya jeshi na waasi wa M23 katika mji Masisi Kati, jimbo la Kivu Kaskazini, yamewahamisha makwao watu 102,000.

Wizara ya mambo ya nje ya Rwanda inadai kuwa eneo lililotwaliwa na waasi wa M23 hivi karibuni lilikuwa kwenye mikono ya wanamgambo wa Kihutu, FDLR, wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda.

Soma pia:Rais wa Kongo afanya mabadiliko makubwa jeshini 

Kwenye taarifa yake, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, alilaani ukosoaji wa jamii ya kimataifa ambayo alisema imeshindwa kulaani kuendelea kukiukwa  kwa mamlaka ya ardhi ya Kongo inayomilikiwa na jamii za Wakongo, wakiwemo Watutsi raia wa Kongo.