1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 10 wauawa Mogadishu

2 Januari 2014

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa jana kwenye hoteli yenye ulinzi mkali katika mji mkuu wa Somalia, Mogadisgu, imefika watu 11, miongoni mwao wakiwemo maafisa wa usalama na raia wa kawaida.

https://p.dw.com/p/1AkGe
Maafisa wa polisi wakikagua mabaki ya sehemu ya jengo la hoteli ya al-Jazeera mjini Mogadishu baada ya mashambulizi.
Maafisa wa polisi wakikagua mabaki ya sehemu ya jengo la hoteli ya al-Jazeera mjini Mogadishu baada ya mashambulizi.Picha: Reuters

Hadi sasa hakuna hakuna kikundi ambacho kimedai rasmi kuhusika na mashambulizi hayo, lakini kundi la al-Shabaab lenye mafungamano na mtandao wa al-Qaida limekuwa likishutumiwa kwa mashambulizi kama hayo.

Hussein Aweys, mwandishi wa habari aliyeko mjini Mogadishu, anazungumzia hali ilivyo baada ya mashambulizi hayo ya jana.

Mwandishi: Daniel Gakuba
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman