1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yousaf kuwa waziri kiongozi mpya wa Scotland

28 Machi 2023

Bunge la Scotland linajiandaa kumuidhinisha Humza Yousaf kuwa waziri kiongozi mpya baada ya kupata ushindi finyu katika kinyang'anyiro cha kumrithi Nicola Sturgeon kama kiongozi wa chama cha Scottish National (SNP).

https://p.dw.com/p/4PMwJ
Schottland Edinburgh | Schottlands Gesundheitsminister Humza Yousaf nach Wahl zum SNP-Parteivorsitzenden
Picha: Jeff J Mitchell/Getty Images

Yousaf aliwabwaga wapinzani wake wawili ndani ya chama hicho jana na kuahidi kuipa nguvu tena  sera ya chama hicho ya kudai uhuru wa Scotland. 

Yousaf mwenye umri wa miaka 37 atakuwa ndio waziri kiongozi wa kwanza mwenye umri mdogo tangu kuundwa kwa bunge la Scotland baada ya mageuzi ya kimajimbo mnano mwaka 1999 na kiongozi wa kwanza wa chama hicho kitaifa kutoka jamii ya walio wachache.

Bunge mjini Edinburgh litapiga kura baadaye kumuidhinisha kiongozi mpya na Yousaf anauhakika wa kumrithi Sturgeon kutokana na chama cha SNP kuwa na wabunge wengi.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW