Xi atoa wito kuzisaidia Urusi na Ukraine kufanya mazungumzo
9 Julai 2024Shirika la habari la China CCTV limemnukuu Xi akisema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuunda mazingira bora na kutoa usaidizi kwa Ukraine na Urusi ili kuanza tena kwa mazungumzo ya moja kwa moja.
Soma pia:Rais wa China Xi Jinping afanya ziara nchini Hungary
CCTV pia imeripoti kuwa Xi amemwambia Orban ni wakati tu ambapo mataifa yenye ushawishi yatakuwa na msukumo wa tija ndipo utakapokuwa mwanzo wa usitishaji haraka wa vita katika mzozo huo.
China ina ushawishi wa kuleta amani kati ya Urusi na Ukraine
Kufuatia mazungumza kati ya Orban na Xi, Orban aliandika ujumbe katika mtandao wa kijamii wa X kwamba China ni taifa lenye ushawishi katika kuunda mazingira ya amani kwenye vita vya Urusi na Ukraine.
Mkutano kati ya Orban na Xi waibua wasiwasi
Marekani imesema ina wasiwasi kuhusu mkutano huo kati ya Orban na Xi, huku msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa John Kirby akisema ziara hiyo haionekani kuwa na tija katika suala la kujaribu kurekebsiha hali nchini Ukraine.