1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Xavi Simons kubakia Leipzig

5 Agosti 2024

Kiungo wa kati wa Paris Saint-Germain Mholanzi Xavi Simons ameongeza muda wa mkopo wake katika RB Leipzig kwa mwaka mwingine akiwapiga chini Bayern Munich.

https://p.dw.com/p/4j8SH
Xavi Simons
Xavi Simons kubakia RB Leipzig kwa msimu mwinginePicha: Michael Weber/IMAGO

 Kiungo wa kati wa Paris Saint-Germain Mholanzi Xavi Simons ameongeza muda wa mkopo wake katika RB Leipzig kwa mwaka mwingine akiwapiga chini Bayern Munich.

Mapema Jumatatu ya tarehe 05.08.2024 klabu yake ya PSG ilithibitisha mkopo huo siku lakini ikasisitiza kwamba mkataba huo "hauna chaguo la kumnunua".

"Paris Saint-Germain inamtakia Xavi msimu mzuri na RB Leipzig," klabu hiyo ilisema katika taarifa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye alitamba na timu yake ya taifa ya Uholanzi kwenye michuano ya Euro 2024 kwa kufunga bao la kwanza katika mechi ya nusu fainali waliyopoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya England pia aliisaidia vya kutosha kupata matokeo mazuri Leipzig msimu uliopita.

Soma zaidi. Conceicao aipa ushindi Portugal kwa bao la dakika za mwisho

Mabao manane na pasi 13 za mabao katika mechi 32 za Bundesliga yalitosha kuteka hisia za vilabu kadhaa vya Ulaya ikiwemo Bayern Munich kuitaka huduma yake.

Xavi Simons
Mchezaji Xavi Simons kubakia kwenye Bundesliga kwa msimu mwinginePicha: Oliver Zimmermann/foto2press/IMAGO

Mkurugenzi mtendaji wa Bayern Max Eberl, ambaye alikuwa katika nafasi hiyo Leipzig wakati klabu hiyo ilipomsajili Simons msimu uliopita, alimsifu Simons kwa kusema ni "mchezaji bora" mwezi uliopita na kuwaahidi miamba hao wa Ujerumani kwamba watajaribu kila kitu kumleta kiungo huyo pamoja na wachezaji wengine kujiunga na Bayern.

Simons alijiunga na PSG mwaka wa 2019 lakini amecheza mechi saba pekee za Ligue 1 akiwa na timu hiyo, akiwa pia amekaa mwaka mmoja PSV Eindhoven.