1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wolfsburg, Ujerumani. Kiongozi wa kampuni la magari la Volkswagen ajiuzulu kutokana na madai ya hongo.

1 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEyb

Kampuni la kutengeneza magari la Volkswagen nchini Ujerumani limesema kuwa limewataka waendesha mashtaka kuchunguza madai ya hongo katika kiwanda chake kingine cha kutengeneza magari aina ya Skoda baada ya taarifa za magazeti kadha nchini Ujerumani kuandika juu ya kashfa hiyo.

Katika hatua ambayo haikutarajiwa , kiongozi wa baraza la wafanyakazi la kampuni ya Volkswagen Klaus Volkert amejiuzulu lakini amekanusha madai ya kuhusika na kashfa hiyo katika kampuni la Skoda. Bwana Volkert, mwenye umri wa miaka 62, amesema kuwa umri ndio sababu yake kubwa ya kujiondoa katika uongozi.

Majarida hayo Spiegel na Focus yamesema kuwa kiongozi wa zamani wa wafanyakazi katika kampuni la skoda , Helmut Schuster amehusika katika hongo kutoka katika makampuni yanayoiuzia vipuri kampuni hiyo ya magari.