Marekani yafunguwa kesi kupinga kufutwa wapigakura Virginia
12 Oktoba 2024Matangazo
Mashitaka hayo yaliyofunguliwa jana mjini Alexandria yanasema kuwa amri iliyotolewa mwezi Agosti na Gavana Glenn Youngkin kutokea chama cha Republican, ambayo inataka kufanyike uhakiki wa kila siku kwenye daftari hilo ili kuwaondowa wapigakura wasio halali, inakinzana na sheria ya uchaguzi ya taifa.
Soma zaidi: Pigo kwa Trump baada ya Matt Bevin kushindwa Kentucky
Sheria hiyo inaamuru kuwa siku 90 kabla ya uchaguzi kusiwe na shughuli zozote kwenye daftari la wapigakura.
Kwa wengi, amri ya gavana wa Virginia ina lengo la kuwaondosha wapigakura wenye historia ya uhamaji na uhamiaji, hasa kutokana na mwenendo wa mgombea urais kupitia Republican, Donald Trump, ambaye ameamua kuzigeuza kampeni zake kuwa na ajenda kubwa dhidi ya wahamiaji.