1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Karibu watu 36,000 wauawa katika Ukanda Gaza

31 Mei 2024

Wizara ya afya katika Ukanda Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema watu wasiopungua 36,284 wameuawa katika eneo hilo katika kipindi cha zaidi ya miezi saba ya vita kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina.

https://p.dw.com/p/4gVam
Mashambulizi | Ukanda wa Gaza, Rafah
Raia katika Ukanda wa Gaza wakiangalia masalia baada ya shambulizi lililofanywa na vikosi vya IsraelPicha: Jehad Alshrafi/dpa/picture alliance

Idadi hiyo inajumuisha takriban vifo 60 katika muda wa saa 24 zilizopita, taarifa ya wizara hiyo imesema.

Watu 82,057 wamejeruhiwa katika Ukanda wa Gaza tangu vita vilipoanza baada ya wapiganaji wa Hamas waliposhambulia eneo la kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, 2023.

Jeshi la Israel limethibitisha leo kuwa vikosi vyake vinaendelea na mashambulizi katika sehemu za kati za mji wa Rafah huku likiwa limeongeza mashambulizi yake katika eneo hilo la kusini mwa Ukanda wa Gaza.