1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wizara ya Afya Gaza yasema vifo vya vita vimefikia 37,296

15 Juni 2024

WIzara ya Afya ya Ukanda wa Gaza inayoendeshwa na Hamas, imesema watu wasiopungua 37,296 wameuawa katika eneo hilo wakati wa vita vya zaidi ya miezi nane kati ya Israel na wapiganaji wa makundi ya Kipalestina.

https://p.dw.com/p/4h5Jp
Vita vya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza
Juhudi za kufikia muafaka kati ya Israel na Hamas wa kusitisha mapigano kufikia sasa zimegonga mwambaPicha: Evad Baba/AFP

Idadi hiyo inajumlisha vifo visivyopungua 30 katika muda wa saa 24 zilizopita, imesema taarifa ya wizara hiyo, na kuongeza kuwa jumla ya watu 85,197 wamejeruhiwa kote Gaza tangu kuanza kwa mzozo huo wa kivita.

Soma pia: Marekani kusitisha oparesheni kwenye gati la misaada Gaza

Juhudi za kufikia muafaka kati ya Israel na Hamas wa kusitisha mapigano kufikia sasa zimegonga mwamba.

Kundi la Kipalestina la Islamic Jihadi, linalopambana sambamba na Hamas huko Gaza, limesema mateka wa Israel wataachiwa tu kama Israel itaondoa vikosi vyake kikamilifu Gaza, na kuwaachiwa wafungwa wote wa Kipalestina wanaozuwiliwa katika magereza ya Israel.