1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Mashambulizi ya Israel ukanda wa Gaza yamewauwa watu 73

8 Januari 2024

Wapalestina 73 wameuwawa na wengine 99 wamejeruhiwa katika muda wa saa 24 zilizopita kutokana na mashambulizi ya vikosi vya Israel yanayoendelea kwenye Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4ayNm
Wapalestina wakikagua majumba yaliyoharibiwa na mashambulizi ya anga ya Israel
Wapalestina wakikagua majumba yaliyoharibiwa na mashambulizi ya anga ya IsraelPicha: Mohammed Dahman/AP Photo/picture alliance

Hayo yameelezwa na wizara ya afya ya Ukanda huo inayoongozwa na kundi la Hamas.

Kwa upande wake jeshi la Israel limesema limewauwa wapiganaji 10 wa kipalestina kusini mwa Gaza katika operesheni iliyofanikiwa kuharibu ghala moja la silaha na kugundua moja ya mahandaki ya maficho.

Soma pia:  Borell aonya Lebanon kuingizwa vitani Mashariki ya Kati

Wakati huo huo ndege na helikopta za Israel zimefanya mashambulizi nchini Lebanon dhidi ya maeneo ambayo jeshi la nchi hiyo linasema yanatumiwa na kundi la Hezbollah.

Hayo yakijiri mawaziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani na Marekani wanaitembelea Mashariki ya Kati kwa mara nyingine kujaribu kutuliza mivutano inayotishia kuutanua mzozo wa Gaza.

Mwanadiplomasia wa Ujerumani Annalena Baerbock anaelekea mjini Ramallah huko Ukingo wa Magharibi kwa mazungumzo na viongozi wa Palestina baada ya kufanya mashauriano na viongozi wa Israel mjini Tel Aviv.