1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Zaidi ya wahudumu 16 wa afya wamekufa Gaza

7 Novemba 2023

Msemaji wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, Christian Lindmeier, amesema zaidi ya wahudumu wa afya 16 wamekufa wakitimiza wajibu wao huko Gaza.

https://p.dw.com/p/4YWKX
Shambulizi la Israel kambi ya wakimbizi ya Al-Maghazi Gaza
Wahudumu wa afya wakimsaidia mhanga wa shambulizi la IsraelPicha: Ashraf Amra/AA/picture alliance

Lindmeier ametoa pia wito wa kusitishwa vikwazo kwa misaada ya vifaa vya matibabu, akisema baadhi ya madaktari wamekuwa wakiwafanyia watu upasuaji, ikiwa ni pamoja na kukatwa viungo bila kutumia ganzi. Israel imekuwa ikitupilia mbali miito ya usitishwaji mapigano huko Gaza.

Aidha, Wizara ya Afya inayodhibitiwa na kundi la Hamas huko Gaza imesema hadi sasa Wapalestinia 10,328 wameuawa huku 4,237 miongoni mwa hao wakiwa ni watoto.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi la Kipalestina UNRWA imesema asilimia 70 ya watu wameyahama makazi yao huko Gaza. Mzozo kati ya Israel na Hamas umetimiza mwezi mmoja leo ambapo pia Waisrael 1,400 waliuawa huku wengine zaidi ya 200 wakichukuliwa mateka.