1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO: Ruksa kwa washirika wetu kuanza kununua chanjo za mpox

23 Agosti 2024

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema washirika wake wanaweza kuanza kununua chanjo za mpox hata kabla ya kuidhinishwa na shirika hilo la Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/4jrUx
Mpox  Chanjo I Chanjo ya Mpox
Mtumishi wa afya akitoa chanjo dhidi ya mpox. Kumekuwa na ongezeko la maambukizi ya mpox hatua inayoyasukuma mataifa kuangazia namna ya kuyadhibitiPicha: Seth Wenig/AP/picture alliance

WHO inachukua hatua hii katika juhudi za kutoa chanjo haraka barani Afrika wakati ambapo maambukizi ya virusi vya mpox yanazidi.

Kwa kawaida asasi kama vile Gavi na UNICEF, zinazozisaidia nchi za vipato vya chini kununua dawa zinaruhusiwa tu kununua chanjo baada ya kuidhinishwa, lakini kanuni zimebadilishwa ili kuanzisha mazungumzo juu ya upatikanaji wa chanjo hizo.

Chanjo za aina mbili kutoka Denmark na Japan zimeshapitishwa na wakaguzi. Kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuia magonjwa, CDC, kimesema baadhi ya chanjo za mpox zilizotolewa kama msaada zinatarajiwa kuwasili barani Afrika wiki ijayo.