1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
TeknolojiaDenmark

Takriban asilimia 16 ya vijana wananyanyasika mitandaoni

27 Machi 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya, WHO limesema takriban asilimia 16 ya watoto wenye umri wa kati ya miaka 11 hadi 15 walikabiliwa na dhulma za mtandaoni mwaka 2022.

https://p.dw.com/p/4eBdk
Vijana wengi wanakabiliwa na unyanyasaji wa mitandaoni Barani Ulaya
Msichana kama anavyoonekana akisononeka wakati akiangalia simu yake ya mkononiPicha: Antonio Guillen Fernández/PantherMedia/IMAGO

Idadi hii ni imeongezeka kutoka asilimia 13 miaka minne iliyopita, limesema WHO katika ukanda wa Ulaya.

Ripoti ya utafiti huo kwa jina ''Mienendo ya kiafya miongoni mwa wanafunzi, iliyotolewa leo na ambayo ilihusisha nchi 44, imesema asilimia 15 ya wavulana na 16 ya wasichana waliripoti kudhulumiwa mitandaoni angalau mara moja katika miezi ya hivi karibuni.

Katika taarifa, mkurugenzi wa WHO katika kanda hiyo ya Ulaya Hans Kluge, amesema ripoti hiyo ni mwamko kwa watu wote kushughulikia dhulma hizo na uonevu, wakati wowote na popote zinapotokea.

Soma pia:Meta, TikTok na X, wabanwa kuhusu usalama mtandaoni

Ripoti hiyo imeongeza kuwa unyanyasaji kupitia mitandao umeongezeka tangu kuzuka kwa janga la Uviko-19, wakati vijana wengi walizidisha matumizi ya mitandao.

Bila kutoa maelezo zaidi, WHO imesema viwango vya juu zaidi vya dhulma hizo za mtandaoni ziliwakumba wavulana nchini Bulgaria, Lithuania, Moldova na Poland, huku vya chini zaidi vikiripotiwa nchini Uhispania.