1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya kituo cha chanjo Gaza yajeruhi watoto 4

Hawa Bihoga
3 Novemba 2024

Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, WHO limesema watoto wanne ni miongoni mwa watu sita waliojeruhiwa hapo jana Jumamosi katika shambulio dhidi ya kituo cha chanjo ya polio kaskazini mwa Gaza.

https://p.dw.com/p/4mXfk
Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkuu wa WHO Tedros Adhanom GhebreyesusPicha: John Macdougall/AFP/Getty Images

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kituo hicho cha afya kilichoshambuliwa kilikuwa katika eneo ambalo lilikubaliwa kusitisha mapigano ili kuruhusu huduma za kiutu ikiwemo utolewaji wa chanjo hiyo ya Polio.

Baadhi ya wafuatiliaji wanasema shambulio hilo huenda likaathiri pakubwa zoezi hilo muhimu ikiwemo kuwazuwia wazazi kupeleka watoto wao wanaohitaji chanjo ya pili.

Soma pia:WHO yapoteza mawasiliano na wafanyakazi katika hospitali ya Gaza

WHO ilianza tena awamu ya pili ya utolewaji wa chanjo kaskazini mwa Gaza hapo jana  baada ya kulazimishwa kuzisitisha huduma kufuatia mashambulizi ya Israel. 

Hata hivyo jeshi la Israel limekanusha madai ya kushambulia kituo hicho cha afya cha Sheikh Radwan kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.