1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

WHO ina wasiwasi wa kuzuka mripuko wa ugonjwa wa polio Gaza

23 Julai 2024

Afisa wa ngazi ya juu wa Shirika la Afya Duniani WHO ameonesha wasiwasi juu ya uwezekano wa miripuko katika Gaza iliyokumbwa na vita baada ya virusi vya ugonjwa wa kupooza kugunduliwa kwenye maji taka

https://p.dw.com/p/4idmD
Polio
WHO ina wasiwasi wa kuzuka mripuko wa ugonjwa wa polio GazaPicha: K.M. Chaudary/AP Photo/picture alliance

Ayadil Saparbekov, ambae ni mkuu wa huduma za dharura wa shirika hilo katika maeneo ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, alisisitiza kuwa "bado hawaja kusanya sampuli za binadamu" kwa hivyo bado haijafahamika ikiwa kuna mtu yeyote aliyeambukizwa virusi hivyo.

Wapalestina watano wauawa kwa droni katika Ukingo wa Magharibi

"Nina wasiwasi sana kuhusu mripuko unaotokea Gaza. Na hii sio polio pekee - miripuko tofauti ya magonjwa ya kuambukiza ambayo inaweza kutokea huko Gaza. Kulikuwa na hepatitis A iliyothibitishwa mwaka jana na sasa tunaweza kuwa na polio.

Lakini juma lililopita mashirika ya Umoja wa Mataifa yalisema Mtandao wa Maabara wa Kimataifa ya Polio ulipata virusi vya polio aina ya pili vilivyotokana na chanjo katika sampuli sita za kimazingira zilizokusanywa kutoka kwa maji taka katika Ukanda wa Gaza mwezi Juni 23.