1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WFP yaanza tena utoaji huduma Sudan

1 Mei 2023

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula Duniani, WFP, Cindy McCain, amesema shirika hilo litaanza tena shughuli za utoaji misaada ya kiutu nchini Sudan, kufuatia mzozo nchini humo kuendelea kupambamoto

https://p.dw.com/p/4QkqI
Flüchtende Sudanesen suchen Zuflucht im Tschad
Picha: Mahamat Ramadane/Reuters

Katika ujumbe aliouandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter, McCain amesema wameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuwa mzozo unaoendelea nchini humo unazidi kuwapelekea mamilioni ya watu kuathirika na njaa.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limekuwa likitahadharisha kwamba mapigano hayo ya Sudan huenda yakaitumbukiza kanda nzima ya Afrika Mashariki katika mzozo wa kiutu.

Mapigano mapya Sudan, UN yatahadharisha hali mbaya ya kiutu

WFP ilikuwa imesitisha huduma zake nchini Sudan kufuatia vifo vya wafanyakazi wake watatu na kujeruhiwa kwa wafanyakazi wake wengine wawili katika shambulizi lililofanywa huko Kabkabiya kaskazini mwa Darfur.