WFP imesitishja ugawaji chakula Yemen
5 Desemba 2023Matangazo
Sababu nyingnie ya hatua hiyo ni kutoelewana na mamlaka ya eneo hilo kuhusiana na namna ya kuwashughulikia watu masikini huko. Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema uamuzi wake umechukuliwa baada ya kushauriana na wafadhili na umekuja baada ya mwaka mmoja wa mazungumzo na kushindwa kupatikanamakubaliano ya kupunguza idadi ya watu inaowasaidia kutoka milioni 9.5 hadi milioni 6.5. Akiba ya chakula katika maeneo yanayodhibitiwa na Wahouthi inakaribia kabisa kumalizika na kurudisha msaada wa chakula katika eneo hilo huenda ikachukua hadi miezi minne, kutokana na kuvurugika kwa mfumo wa usambazaji chakula. Mamilioni ya watu bado wanategemea moja kwa moja msaada wa kibinadamu nchini Yemen.