1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSomalia

WFP: Baa la njaa limeepukwa Somalia, lakini halijamalizika

18 Januari 2023

Mkuu wa Mpango wa Chakula Duniani, WFP David Beasley amesema msaada ya kiutu kutoka nchi kama Marekani na Ujerumani umesaidia kuepusha kwa muda baa la njaa nchini Somalia, lakini tatizo halijakwisha.

https://p.dw.com/p/4MOBr
Dürre und Trockenheit am Horn von Afrika
Picha: Claire Nevill/AP Photo/picture alliance

Mkuu wa Mpango wa Chakula Duniani, WFP  David Beasley amesema msaada ya kiutu kutoka nchi kama Marekani na Ujerumani umesaidia kuepusha kwa mudabaa la njaa nchini Somalia, ingawa hawezi kusema kuwa tatizo hilo limekwisha.

Amesema nchi za Pembe ya Afrika zimekabiliwa na ukame usio na kifani kwa miaka kadhaa, na kuongeza kuwa shirika lake lilikuwa likijiandaa kutangaza baa la njaa katika ukanda kabla ya wahisani kuingilia.

Beasley ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa bado kitisho cha janga hilo kinaweza kutokea kwa sababu hali ya uhaba mkubwa wa chakula ipo Somalia.

Afisa huyo ambaye zamani alikuwa gavana wa jimbo la South Carolina nchini Marekani ameweza kutumia ushawishi wake wa kisiasa kukusanya msaada wa Washington, chini ya utawala wa rais Donald Trump na pia wa Joe Biden.

Mwezi uliopita Marekani ilitangaza msaada mpya wa dila milioni 411 kwa ajili ya kupambana na upungufu wa chakula nchini Somalia.