Mali: Wenye itikadi kali wadai kuwauwa walinzi wa amani
14 Juni 2023Taarifa hiyo imetolewa katika tovuti yake ya propaganda ya All-Zallaqa.Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali- MINUSMA, kimesema shambulio tata lililohusisha kiripuzi na shambulizi la moja kwa moja vililenga askari waliokuwa katika doria karibu na mji wa Ber, katika mkoa wa Timbuktu.
Mali imekuwa ikikabiliana na mzozo wa kisiasa na kiusalama tangu mwaka 2012 pale ambapo waasi wanaotaka kujitenga na makundi ya itikadi kali yalipozuka kaskazini, na baadaye kuenea katika nchi jirani za Niger na Burkina Faso.
Soma pia: Mwanajeshi wa pili wa kulinda amani Mali, afariki
Katika ripoti yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo litapiga kura Juni 29 kuhusu kurefusha moja ya mpango hatari zaidi wa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa, katibu mkuu wa umoja huo, Antonio Guterres alitoa wito wa "kuundwa upya" kwa mamlaka ya kikosi hicho ambacho kilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2013.