1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ulinzi wa Urusi atembelea mstari wa mbele wa vita

4 Machi 2023

Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu, amefanya hii leo ukaguzi wa vikosi kwenye uwanja wa mapambano mashariki mwa Ukraine, wakati mapigano yakiendelea viungani mwa mji wa mashariki wa Bakhmut.

https://p.dw.com/p/4OFZt
Russland Verteidigungsminister Sergej Schoigu verkündet Umbau der Armee
Picha: Russian Defence Ministry/AP/picture alliance

Wizara ya ulinzi imesema leo kuwa Shoigu alikagua kituo cha uratibu katika mkoa wa kusini wa Donetsk, bila kutaja mahala rasmi au wakati kamili wa ziara hiyo.

Katika video iliyochapishwa na wizara hiyo, Shoigu ameonekana akitoa medali kwa wanajeshi wa Urusi.

Soma: Zelensky arejea wito kwa Ukraine kupatiwa silaha nzito

Maafisa wakuu wa jeshi la Urusi wamekuwa wakitembelea mara chache maeneo ya uwanja wa vita tangu walipoivamia Ukraine mwaka mmoja uliopita.

Shoigu, ambaye amehudumu kama waziri wa ulinzi tangu mwaka 2012, amekuwa akikosolewa vikali kwa utendaji wake katika vita hivyo.