Waziri wa ulinzi wa Israel, Yoav Gallant aelekea Marekani
23 Juni 2024Matangazo
Awali Gallant amesema "atajadili maendeleo huko Gaza na Lebanon, na kuapa kwamba wako tayari kwa hatua yoyote ambayo inaweza kuhitajika huko Gaza, Lebanon na katika maeneo ya ziada.
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alielezea matumaini ya maendeleo ya haraka katika kuruhusu tena utoaji wa silaha kutoka kwa Marekani, mshirika mkuu wa Israel ambao alisema umeshuka kwa kasi katika miezi ya hivi karibuni. Rais wa Marekani Joe Biden amekuwa akitofautiana na kiongozi huyo mkongwe wa mrengo wa kulia wa Israel kuhusu kuongezeka kwa idadi ya vifo vya raia Gaza.