1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ujerumani Baerbock afuta ziara ya Pasifik

15 Agosti 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock ameifuta ziara yake ya wiki nzima ya kanda ya Pasifiki baada ya ndege aliyokuwa akiitumia kupata hitilafu ya kiufundi mara mbili ikiwa njiani kuelekea Sydney

https://p.dw.com/p/4VCkg
VAE,  Abu Dhabi | Deutsche Regierungsmaschine gestrandet auf dem Weg nach Australien
Picha: Florian Gaertner/photothek/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock ameifuta ziara yake ya wiki nzima iliyojumuisha kuitembelea Australia, New Zealand na kisiwa cha Fiji baada ya ndege aliyokuwa akiitumia kupata hitilafu ya kiufundi mara mbili ikiwa njiani kuelekea Sydney.

Deutsche Außenministerin Annalena Baerbock im Gespräch mit DW
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani BaerbockPicha: DW

Ndege hiyo ya serikali aina ya Airbus chapa 340 ililazimika kukatisha safari mara mbili baada ya kuruka kutoka mji wa Abu Dhabi ilikosimama kwa muda ikiwa imembeba mwadiplomasia huyo wa Ujerumani kuelekea Australia.

Bibi Baerbock amesema licha ya kufanyiwa matengenezo chombo hicho kimeshindwa kuendelea na safari na kwa hiyo uamuzi umefikiwa wa kuifuta ziara yake kwenye kanda ya bahari ya bahari Hindi na Pasifiki.

Hilitafu zinazohusisha ndege za serikali ya Ujerumani limekuwa jambo linalojirudia. Kufuatia kisa cha Abu Dhabi, jeshi la Ujerumani limetangaza kuziondoa mapema ndege mbili chapa A340  katika orodha ya zile zinazotumika kuwasafirisha viongozi. Hapo awali iliamuliwa kuwa ndege hizo zitatumika hadi mwishoni mwa mwaka ujao.