Waziri Baerbock aihimiza China kuiambia Urusi isitishe vita
14 Aprili 2023Mwanadiplomasia huyo wa Ujerumani ametoa matamshi hayo baada ya kukutana na mwenzake wa China Qin Gang ambapo wamejadili pamoja na mambo mengine, suala la haki za binadamu na kutanuka kwa mvutano juu ya kisiwa cha Taiwan.
Soma pia: Nchini China, Baerbock asema maoni ya Macron ni ya Ulaya
Ama kuhusu dhima ya China katika kukomesha vita nchini Ukraine Bibi Baerbock amesema; "Ninatumia ziara yangu pia kuirai China, kama mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kupigania amani ulimwenguni na kusaidia kuhakkisha kwamba vita vya kutisha vya Urusi vinafikia mwisho"
Katika miezi ya karibuni China imechukua jukumu la kutaka kuwa mpatanishi wa mzozo wa Ukraine lakini mataifa ya magharibi yana mashaka na dhamira ya Beijing iliyo mshirika mkubwa wa Moscow.