Waziri wa mambo ya nje wa Saudia ziarani Syria
18 Aprili 2023Katika miezi ya hivi karibuni, viongozi wa nchi kadhaa za kiarabu, wamekuwa wanasogea kwa rais Bashar al-Assad wa Syria ambaye hapo awali alitengwa kisiasa tangu kuanza kwa mgogoro wa nchini mwake.
Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Faisal bin Farhan anafanya ziara nchini Syria muda mfupi tu baada ya waziri wa mambo ya nje wa Syria Faisal Mekdad kufanya ziara nchini Saudi Arabia.
Soma pia: Mataifa ya Kiarabu yaujadili mgogoro wa Syria
Kwenye mkutano wao mawaziri hao walijadili njia zinazolazimu kuchukuliwa ili kuondosha kutengwa kwa Syria. Wiki iliyopita viongozi wa nchi za kiarabu walikutana kwenye mji wa Saudi Arabia wa Jeddah kujadili njia za kuumaliza muda mrefu wa kutengwa kwa Syria kidiplomasia.
Saudi Arabia ilivunja uhusiano wa kibalozi na Syria mnamo mwaka 2012 na pia iilisimama mstari wa mbele katika harakati za kutaka kuangushwa utawala wa Assad.