Antony Blinken atarajiwa kuwasili Moldova
29 Mei 2024Katika ziara hiyo atakutana na rais Maia Sandu na analenga kuimarisha uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa Ukraine katika mataifa yote washirika wa Jumuiya ya kujihami ya NATO na mataifa jirani.
Ziara hiyo inakuja wakati Ukraine ikijaribu kuzuia mashambulizi yaliyoongezeka ya Urusi kwenye maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo, huku rais Vladmir Putin akizionya nchi za Magharibi kwamba kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za mataifa hayo kushambulia ndani ya ardhi yake ni hatua inayoweza kuchochea vita vya dunia.
Ukraine imesema Urusi inazidisha mashambulizi nchini humo
Baadae wiki hii atakwenda Prague kushiriki mkutano usiokuwa rasmi wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa NATO wa maandalizi ya mkutano wa kilele wa viongozi wakuu utakaofanyika Julai.