1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Antony Blinken awasili Moldova kwa mazungumzo na rais Sandu

29 Mei 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amewasili Moldova ambako atakutana kwa mazungumzo na rais wa nchi hiyo Maia Sandu.

https://p.dw.com/p/4gQkp
Ukraine |Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: Brendan Smialowski/AP/dpa/picture alliance

Ziara hiyo inalenga kuonesha uungaji mkono wa Marekani wa mataifa washirika wake wa Magharibi katika wakati ambapo wasiwasi unaongezeka kuhusu kuongezeka kwa nguvu za Urusi kwengineko.

Moldova iko katikati ya Ukraine na Romania ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya na Urusi imeweka wanajeshi wake katika jimbo la Moldova lililojitenga na Transnistria.

Erdogan asema Umoja wa Ulaya utakwamisha kujiunga kwa Ukriane, Moldova

Urusi imelitumia eneo hilo kujipatia ushindi kwenye uwanja wa vita nchini Ukraine. Blinken anatarajiwa kutangaza msaada mkubwa kwa Moldova,kwa mujibu wa  naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayehusiana na masuala ya Ulaya, Jim O'Brien.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW