Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini aelekea Urusi
29 Oktoba 2024Shirika la habari la Korea Kaskazini limesema ujumbe ulioongozwa na Chie uliondoka jana kwa ziara rasmi nchini Urusi, bila kufafanua.
Choe ameelekea Moscow wakati Jumuiya ya Kujihami ya NATO ikiungana na Korea Kusini na Marekani katika kuthibitisha kuwa Korea Kaskazini imepeleka wanajeshi nchini Urusi.Inasema vikosi vya jeshi la Korea Kaskazini vilipelekwa katika eneo la Urusi la Kursk kwenye mpaka na Ukraine. Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema Washington haitaweka vizuizi vipya kwa Kyiv kutumia silaha za Kimarekani kama Korea Kaskazini itaingia katika vita vya Moscow dhidi ya Kyiv. Ilisema Korea Kaskazini imepeleka askari 10,000 mashariki mwa Urusi kwa ajili ya mafunzo.
Soma pia: Kansela Olaf Scholz wa ujerumani ahofia kutumwa wanajeshi wa Korea kaskazini nchini Ukraine
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Mark Rutte amesema kuongezeka kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Urusi na Korea Kaskazini ni kitisho kwa usalama wa eneo zima la Indo Pasifiki pamoja na kanda ya Ulaya, mataifa ya Caucasus na Asia ya Kati.