Ziara ya utatanishi.
7 Mei 2009Waziri wa mambo ya nje wa Israel Avigdor Liebermann leo ameanza ziara nchini Ujerumani kituo cha mwisho katika ziara yake barani Ulaya.
Waziri Lieberman ambae ni kiongozi wa chama chenye mrengo mkali wa kizalendo nchini Isreal- Beiteinu aliwasili mapema leo mjini Berlin na amekutana na wajumbe wa kamati ya bunge la Ujerumani inayoshuhgulikia masuala ya mambo ya nje.
Waziri Lieberman amewasili nchini Ujerumani baada ya kuzuru,Italia, Ufaransa,Umoja wa Ulaya na Jamhuri ya Czech.
Waziri huyo kwa mara nyingine amepinga suluhisho la nchi mbili badala yake amezungumzia alichoita kiwanda cha amani ambacho hadi leo hakijazaa matunda bali kimesababisha fedha zipotee.
Hatahivyo baada ya mazungumzo yake na wajumbe wa kamati ya masuala ya nje ya bunge la Ujerumani mjini Berlin, anatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier na waziri wa mambo ya ndani Wolfgang Schauble.
Hapo awali mwanasiasa huyo wa Israel alitembelea kumbukumbu ya maangamizi ya wayahudi mjini Berlin.
Mwandishi :A.Mtullya /AFPE
Mhariri:M.Abdul-Rahman