1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza awasili Rwanda

5 Desemba 2023

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza ,James Cleverly awasili Rwanda kwa ajili ya kufanikisha juhudi mpya ya kuwahamishia wahamiaji waliokwama Uingereza nchini humo.

https://p.dw.com/p/4Zobo
UK Treffen der Konversativen Partei in Manchester | Aussenminister James Cleverly
Picha: Toby Melville/REUTERS

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza James Cleverly amesema makubaliano mapya baina ya nchi yake na Rwanda kuhusu wahamiaji haramu, yatakahakikisha kwamba watu waliohamishiwa katika nchi hiyo ya Afrika, hawatopelekwa katika nchi nyingine yeyote ambako wanaweza kukabiliwa na mateso. Waziri huyo aliyewasili leo nchini Rwanda amesema mkataba huo wa kihistoria waliosaini na Rwanda unazingatia sheria ya kimataifa naunahakikishakwamba waliopelekwa Rwanda chini ya makubaliano hayo ya ushirikiano hawatokuwa katika hatari ya kupelekwa kokote ambako uhuru au maisha yao yatakuwa hatarini. Juhudi hizi mpya za serikali hiyo ya kihafidhina ya Uingereza zimekuja baada ya mahakama ya juu nchini humo mwezi uliopita kuuzuia mpango huo ambao umetajwa tangu mwanzo kwenda kinyume na sheria.