1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaChina

Waziri wa biashara wa Marekani afanya ziara China

28 Agosti 2023

Waziri wa biashara wa Marekani Gina Raimondo anatarajiwa kufanya mkutano na mwenzake wa China katika ziara ya Beijing inayolenga kupunguza msuguano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani.

https://p.dw.com/p/4VdGf
Waziri wa biashara wa China Gina Raimondo
Waziri wa biashara wa China Gina Raimondo (Kushoto)Picha: Andy Wong/REUTERS

Ziara yake - itakayodumu hadi Jumatano - ni moja kati ya mfululizo wa safari zilizofanywa na maafisa wa Marekani kuelekea China katika miezi ya hivi karibuni.

Raimondo aliwasili Beijing jana na alikutana na mkurugenzi wa wizara inayohusika na biashara kanda ya Amerika ya Kaskazini na Oceania Ling Feng.

Waziri huyo wa biashara wa Marekani pia atasafiri hadi mji wa kibiashara wa Shanghai.

Uhusiano kati ya Marekani na Beijing umedorora katika miaka ya hivi karibuni, huku vikwazo vya kibiashara vya Washington vikiwa moja ya sababu ya kutoelewana na China.