Waziri afutwa kazi Brazil kufuatia kashfa za unyanyasaji
7 Septemba 2024Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amemfuta kazi waziri wa haki za binadamu Silvio Almeida, kufuatia madai ya kuwanyanyasa kingono wanawake kadhaa, akiwemo waziri mwenzake. Kashfa hiyo iliyozua ghadhabu nchini Brazil ni ya kwanza na ya aina yake kumhusisha waziri katikaserikali ya Lula tangu kiongozi huyo mkongwe wa siasa za mrengo wa kushoto aliporejea madarakani mwaka jana.
Taarifa ya ofisi ya rais imesema kuwa "rais anaona ni jambo lisilofaa kuendelea kumweka waziri ofisini kwa kuzingatia aina ya tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia," ilisema taarifa hiyo.Brazil yaapa kuilinda demokrasia
Tovuti moja ya habari nchini humo ya Metropoles ilisema kuwa shirika la masuala ya wanawake la Me Too Brazil, lilipokea malalamiko dhidi ya waziri huyo kutoka kwa wanawake kadhaa.
Mmoja ya wanawake waliozungumza dhidi ya Almeida alikuwa ni waziri wa usawa wa Brazil Anielle Franco. Anielle alichapisha ujumbe kwenye ukurasa wa Instagram akiwashukuru watu kwa kuwaunga mkono katika tuhuma hizo.Lula: Ujumbe wangu kwa Brazil ni matumaini na ujenzi
Miongoni mwa wanawake wengine waliowasilisha malalamiko ni Isabel Rodrigues, profesa na mgombea wa baraza la jiji katika manispaa ya jimbo la Sao Paulo. Isabel amemshutumu Almeida kwa kumnyanyasa kingono mwaka 2019.Raia wa Brazil wapiga kura katika uchaguzi mkuu wa kumchagua rais mpya
Polisi wa shirikisho wamesema kuwa wanayachunguza madai hayo huku tume ya maadili ya rais nayo ikianzisha uchunguzi.
Almeida, mwanasheria na profesa wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 48, amekanusha madai hayo na kudai kuwa yanalenga kumchafua. Amesema kupitia ujumbe wa vidio kwenye mitandao ya kijamii kwamba madai hayo ni "uzushi mtupu".