1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mpya wa ulinzi Ujerumani Boris Pistorius aapishwa

19 Januari 2023

Waziri mpya wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius ameapishwa na kuchukua rasmi wadhfa huo Alhamisi 19.01.2023

https://p.dw.com/p/4MPwM
Deutschland neuer Verteidigungsminister Boris Pistorius
Picha: Matthias Balk/dpa/picture-alliance

Kuapishwa kwa Pistorius kunafanyika wakati ambapo kuna mjadala wa iwapo Ujerumani inastahili kuitumia Ukraine zana zaidi nzito za kisasa. Rais Frank-Walter Steinmeier amekabidhi cheti cha uteuzi Pistorius, ambaye alikuwa anahudumu kama waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Lower Saxony.

Waziri anayeondoka Christine Lambrecht aliyejiuzulu akisingizia ukosoaji kutoka kwa vyombo vya habari, amepokea pia cheti cha kuachishwa kazi. Pistorius anaingia afisini wakati ambapo Ukraine imetoa wito kwa marafiki zake wa nchi za Magharibi kuharakisha na kuipa misaada ya silaha nzito na mifumo ya kujilinda angani.

Ukraine imesema Waukraine wanapoteza maisha kutokana na mazungumzo ya yanayokwenda kwa kasi ya kobe yanayofanywa na nchi zinazolenga kuisaidia.