1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Ukraine ziarani Japan

19 Februari 2024

Waziri Mkuu wa Ukraine, Denys Shmyhal, amewasili hii leo nchini Japan kujadili kuhusu ujenzi wa Ukraine baada ya vita. Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida amesema wataendelea kuiunga mkono Ukraine.

https://p.dw.com/p/4cYyW
Tokyo, Japan | Waziri Mkuu wa Ukraine na Denys Shmyhal na mwenzake wa Japan Fumio Kishida
Waziri Mkuu wa Ukraine na Denys Shmyhal na mwenzake wa Japan Fumio Kishida, katika zoezi la utiaki saini mkataba baina ya nchi hizo mbiliPicha: Kazuhiro Nogi/Pool Photo/AP/picture alliance

Wakati uvamizi wa Urusi uliendelea nchini Ukraine, Japan imeahidi msaada wa kifedha wenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 10, hii ikiwa ni ishara ya mshikamano kwa Kyiv kwa kuwa nchi hiyo haiwezi kutoa msaada wa moja kwa moja wa kijeshi, kwa sababu ni marufuku nchini humo kusafirisha silaha.

Soma pia:Zelensky ahimiza msaada zaidi kwa ukraine, mkutano wa Munich

Mwezi Desemba mwaka jana, Japan ilichukua uamuzi wa kihistoria wa kulegeza sheria zake za usafirishaji wa silaha lakini bado kuna vikwazo vya kusafirisha silaha kwa nchi zilizomo kwenye vita. Waziri mkuu wa Ukraine amesema nchi yake kamwe haitasahau msaada wa Japan.