SiasaUingereza
Sunak kuimarisha mpango wake wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda
14 Desemba 2023Matangazo
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amewaambia wanahabari kwamba mara kwa mara amekuwa wazi kama walivyokuwa mawaziri wote kwamba kama kuna njia ambazo sheria hiyo inaweza kuboreshwa na kudumisha ushiriki wa Wanyarwanda katika mpango huo, bila shaka wanaweza kuzingatia hilo.
Mswada huo wa dharura na uliochapishwa wiki iliyopita, ni jibu la Sunak kwa uamuzi wa mahakama ya juu kwamba sera iliyotumia ilikuwa kinyume cha sheria.
Mswada huo utakapopitishwa, utawalazimisha majaji kuichukulia Rwanda kama nchi ya tatu salama na pia unapendekeza kuwapa mawaziri wa Uingereza mamlaka ya kupuuza sehemu za sheria za kimataifa na Uingereza za haki za binadamu.