1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Slovakia amepigwa risasi na kujeruhiwa

15 Mei 2024

Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico amepigwa risasi leo na kujeruhiwa tumboni muda mfupi baada ya kumaliza kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri.

https://p.dw.com/p/4ftab
Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico
Waziri Mkuu wa Slovakia Robert FicoPicha: Petr David Josek/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico amepigwa risasi leo na kujeruhiwa tumboni muda mfupi baada ya kumaliza kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri. Duru kutoka nchini humo zinasema shambulio hilo limetokea kwenye mji wa Handlova ulio kiasi kilometa 190 kaskazini magharibi mwa mji mkuu Bratislava.

Soma:Robert Fico asema Ukraine inadhibitiwa na Marekani 

Kiongozi huyo tayari amekimbizwa hospitali kwa matibabu na mshambulizi amekamatwa. Polisi ililazimika kuwaondoa watu kwenye kituo cha utamaduni ambako kikao cha serikali kilichoongozwa na Fico kilikuwa kinafanyika.

Salamu za pole zimeanza kumiminika kutoka kwa viongozi barani Ulaya wengi wakilaani mkasa huo.

Rais Zuzana Caputova wa Slovakia amesema ameshtushwa na shambulio hilo alilolitaja kuwa la kikatili na amemtakia Fico afua ya mapema. Viongozi wengine akiwemo kansela Olaf Scholz wa Ujerumani, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na marais wawili wa Umoja wa Ulaya wamelaani kisa hicho.