Waziri mkuu wa Japan aapa kuilinda anga ya nchi hiyo
24 Septemba 2024Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida ameapa kuiteta kikamilifu nchi yake baada ya ndege ya doria ya Urusi kuingia katika anga yake.
Akizungumza na vyombo vya habari vya Japan mjini New York nchini Marekani, Kishida alitaja tukio hilo kuwa la ''kusikitisha'' na kuongeza kuwa watalinda ardhi, maji na anga ya Japan.
Hapo jana, waziri wa ulinzi wa Japan Minoru Kishida alithibitisha kuwa ndege hiyo ya doria ya Urusi aina ya Il-38 ilikiuka anga yao katika eneo la kaskazini mwa Kisiwa cha Rebun, Hokkaido, mara tatu.
Soma: Japan, Korea Kusini zatangaza vikwazo vipya dhidi ya Urusi
Kihara amewaambia waandishi habari kuwa jeshi la nchi hiyo lilijibu tukio hilo kwa kutuma ndege za kivita kushika doria pamoja na kutoa onyo kupitia redio huku akilitaja kuwa uvamizi wa kwanza uliothibitishwa tangu mwaka 2019.
Waziri huyo ameongeza kuwa wamewasilisha malalamiko kwa serikali ya Urusi kupitia njia za kidiplomasia na kuihimiza kuzuia kutokea tena kwa tukio kama hilo.