1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Iraq afanya mazungumzo na Rais wa Iran

11 Septemba 2024

Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia al Sudani, amekutana na Rais wa Iran Masoud Pezeshkian mjini Baghdad ambako kwa pamoja wamesema serikali zao zinapinga hatua yoyote ya kutanua vita kati ya Israel na Hamas.

https://p.dw.com/p/4kWDS
 Mohammed Shia al Sudani | Masoud Pezeshkian
Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia al Sudani(kulia) akiwa na Rais wa Iran Masoud Pezeshkian(kushoto)Picha: Murtadha Al-Sudani/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia al Sudani, amekutana na Rais wa Iran Masoud Pezeshkianmjini Baghdad ambako kwa pamoja wamesema serikali zao zinapinga hatua yoyote ya kutanua vita kati ya Israel na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza. Waziri mkuu huyo wa Iraq, amesema kufuatia hali ilivyo katika kanda hiyo wamejadili mambo mengi kuhusu umuhimu wa kuwepo uthabiti, aliosema unakabiliwa na kitisho cha matumizi ya nguvu kinachofanywa na Israel Ukanda wa Gaza. Rais Pezeshkian wa Iran pia amefahamisha kwamba, amesaini mikataba 14 na Iraq ya kutanuwa ushirikiano.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW