1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Waziri Mkuu wa India Modi aelekea Moscow, Vienna wiki ijayo

4 Julai 2024

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, wiki ijayo atafanya ziara nchini Urusi kwa mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin. Hilo limetangazwa na wizara ya mambo ya nje ya India.

https://p.dw.com/p/4hsEN
India | Narendra Modi
Ziara ya Modi mjini Moscow kuwa ishara maalum ya kuthamini uhusiano kati ya India na UrusiPicha: Narinder Nanu/AFP/Getty Images

Ziara hiyo rasmi mnamo Julai 8 na 9 inakuja muda mfupi baada ya Modi kuchaguliwa tena kuwa waziri mkuu wa India. Viongozi hao wawili, Modi na Putin wanatarajiwa kujadiliana zaidi kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya Urusi na India, pamoja na masuala ya kisiasa ya kimataifa na kikanda. Hii ni kulingana na huduma ya vyombo ya habari ya ikulu ya Kremlin.

Soma pia: Urusi yashtumu nchi za Magharibi kuiwekea India shinikizo

Vyombo vya habari vya Urusi vimeelezea ziara ya Modi kuwa ishara maalum ya kuthamini uhusiano kati ya India na Urusi. Ziara hiyo itakuwa ya pili kwa Modi nje ya nchi baada ya kuchaguliwa tena kama waziri mkuu, baada ya kuhudhuria mkutano wa kilele wa G7 nchini Italia katikati ya mwezi Juni.