MigogoroHungary
Orban aufananisha Umoja wa Ulaya na Umoja wa Sovieti
24 Oktoba 2024Matangazo
Waziri Mkuu Orban amesema hayo alipotoa hotuba kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Uasi wa Hungary dhidi ya uvamizi wa Wasovieti, ambao hata hivyo ulidhibitiwa vikali na wanajeshi wa Urusi.
Kribu watu 3,000 waliuliwa na 20,000 walijeruhiwa.
"Kwetu sisi, somo la 1956 ni kwamba lazima tupiganie jambo moja tu: kwa ajili ya Hungary na kwa uhuru wa Hungary," aliwaambia maelfu ya watu katika mkutano wa hadhara huko Budapest.
Orban anayefahamika kwa kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na Rais Vladimir Putin wa Urusi kuliko kiongozi mwingine yoyote wa Ulaya, amekuwa akiukosoa umoja huo kutokana na kuendelea kuiunga mkono Ukraine inayopigana na Urusi.