1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGeorgia

Waziri mkuu wa Georgia aapa kutokomeza upinzani

5 Desemba 2024

Waziri Mkuu wa Georgia Irakli Kobakhidze ameapa leo kuutokomeza upinzani aliouita wa kifashisti nchini humo na kuzidisha kampeni kali ya serikali dhidi ya wapinzani wake.

https://p.dw.com/p/4no3Y
Maandamano | Tbilisi
Mwandamanaji akikabiliana na polisi wakati wa maandamano yaliyofanyika nje ya Jengo la Bunge baada ya Waziri Mkuu Irakli Kobakhidze kusema kuwa nchi hiyo itasimamisha mazungumzo juu ya azma yake ya kujiunga na Umoja wa Ulaya hadi 2028.Picha: Yegikov Mikhail/ITAR-TASS/IMAGO

Kauli yake ameitoa katikati ya maandamano makubwa ya wanaouunga mkono Umoja wa Ulaya yakiingia wiki ya pili.

Kobakhidze amewaambia waandishi wa habari kwamba watafanya kila linalohitajika kutokomeza kabisa ufashisti wa kiliberal nchini humo.

Soma pia: Waandamanaji Georgia wakabiliana na polisi

Waziri huyo mkuu ameongeza kuwa mchakato huo tayari umeanza na kwamba hatua zilizopigwa hivi karibuni zinaashiria mwanzo wa mwisho wa ufashisti wa kiliberali nchini humo, akitumia lugha inayofanana na ile inayotumiwa na Ikulu ya Urusi Kremlin kuwalenga wapinzani wake wa kisiasa.

Kobakhidze, pia alitoa wito kwa wazazi kuwalinda watoto wao kutokana na ushawishi wa vituo vya ufashisti wa kiliberali akimaanisha waandamanaji wenye umri mdogo ambao wanashiriki katika maandamano ya usiku katika barabara za Tbilisi.

Matamshi hayo yanatolewa siku moja baada ya maafisa wa polisi waliojifunika nyuso zao kuvamia makao makuu kadhaa ya chama cha upinzani na kuwakamata viongozi wa upinzani.