1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu Truss asisitiza hang'oki

Iddi Ssessanga19 Oktoba 2022

Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss amejielezea kuwa mpiganaji na siyo mwepesi wa kukata tamaa, wakati akikabiliana na upinzani wenye uhasama na hasira kutoka chama chake cha Conservative.

https://p.dw.com/p/4IQml
Liz Truss, Premierministerin von Großbritannien
Picha: House Of Commons/PA Wire/dpa/picture alliance

Truss ameliomba radhi bunge na kukiri kuwa alifanya makosa katika muda mfupi aliokaaa madarakani, lakini sura za huzuni za wabunge wa Conservative waliokuwa nyuma yake katika baraza la bunge la wawakilishi ziliashiria kwamba Truss anakabiliwa na mapambano makuwa kunusuru kazi yake. 

Truss amehudhuria kikao chake cha kwanza cha maswali ya Waziri Mkuu tangu waziri mpya wa fedha Jeremy Hunt alipouchana mpango wa kupunguza kodi uliozinduliwa na serikali yake mpya chini ya mwezi mmoja uliopita.

Licha ya kuliomba radhi bunge, waziri mkuu huyo amesisitiza kuwa kwa kubadili mwelekeo, alikuwa amewajibika na kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya utulivu wa uchumi wa taifa.

"Nimeweka wazi kwamba naomba msamaha na kwamba nimefanya makosa. Lakini jambo sahihi kufanya katika mazingira hayo ni kufanya mabadiliko ambayo nimefanya na kuendelea kuwatumkia watu wa Uingereza.

Soma pia:Truss aomba radhi kwa makosa lakini hatazamii kujiuzulu

Bwana Spika, tumeshughulikia suala la bei za nishati. Tumewasadia watu msimu huu wa baridi, na nitaendelea kufanya hivyo," alisema Truss mbele ya bunge.

Keir Starmer
Mbunge wa chama cha Labour Keir StarmerPicha: House Of Commons/dpa/picture alliance

Labour washinikiza Truss aachie ngazi

Wakati Truss akizungumza, baadhi ya wabunge walikuwa wanapiga kelele kumtaka ajiuzulu. Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour, Keir Starmer, alisema uaminifu wa kiuchumi wa chama cha Conservative ulikuwa umetoweka baada ya mipango ya waziri mkuu kuishia kuwa janga, na kuhoji kwa nini waziri mkuu huyo bado hajajiuzulu.

"Bwana Spika, mamlaka pekee aliowahi kuwa nayo ni kutoka kwa wajumbe wa chama chake, ilikuwa na mamlaka iliojengwa kwenye uchumi wa njozi." Alisema Starmer.

"Nnchi haijapata chochote zaidi ya kuharibiwa kwa uchumi na kuporomoka kwa chama cha Conservative. Kila alichokiwakilisha kimeondoka, sasa kwa nini yeye bado yuko hapa?" Alihoji bungeni.

Mpango wa kupunguza kodi usio na ufadhili ambao serikali ya Truss iliutangaza Septemba 23, ulisababisha vurugu kwenye masoko ya fedha, kuporomosha thamani ya sarafu ya pauni na kupandisha gharama za ukopaji wa serikali ya Uingereza.

Soma pia:Jeremy Hunt afuta mipango ya kupunguzwa kodi

Benki Kuu ya England ililaazimika kuingilia kati kuzuwia mzozo huo kusambaa kwenye sekta nyingine ya kiuchumi na kuiweka hatarini mifuko ya pensheni.

Akikabiliw ana shinikizo kubwa, Truss alimfuta kazi mshirika wake wa karibu Kwasi Kwarteng kama waziri wa fedha, na nafasi yake kumpa waziri wa siku nyingi Jeremy Hunt.

Siku ya Jumatatu, Hunt alitangaza mabadiliko makubwakatika mpango wa awali ambapo aliondoa karibu vipengele vyote muhimu vinavyohusu makato ya kodi, pamoja na sera yake muhimu kuhusu nishati na ahadi zake za kutokuwepo na punguzo lolote la matumizi.

Wakati ambapo kura za maoni ya wapigakura zikikipa chama cha Labour uongozi mkubwa na unaouidi kuongezeka, wahafidhina wengi wanaamini sasa kwamba tumaini lao pekee la . Lakini waziri mkuu huyo amesisitiza kuwa haachii ngazi, na wabunge wamegawika kuhusu namna ya kumuondoa.

Chanzo: Mashirika